Monday 4 June 2007

Yaliyomo katika Petitions Maalum

Muhtasari: Ukiweza kuchangia yale yanayoenda kinyume na Vyombo vya utendaji vya kiserikali - NI KATIKA KUISAIDIA NCHI NA SERIKALI - Lazima tujenge uaminifu, ubora na uwajibikaji katika serikali.

Changia katika petition hii..

Sisi watanzania tuishio Uingereza tunapinga utaratibu mpya uliotungwa na TBS kwamba katika kuhakikisha magari yanayasafirishwa kwenda Tanzania yakaguliwe ubora wa kuwepo barabarani kwa kufanyiwa ukaguzi na kampuni moja tu.


Kampuni ya WTM UTILITY SERVICES haina historia wala uzoefu wowote wa kukagua magari iweje wapewe mkataba huu? Tunataka kufahamishwa vigezo vilivyotumika kuwapatia WTM UTILITY SERVICES mkataba huu.

Mfumo wa kukagua magari na viwango vya magari ya Uingereza ni vya hali ya juu, Kwa kawaida gari zote zilizopo nchini Uingereza zinatakiwa ziwe na ubora wa kiwango fulani ili kuendeshwa kihalali, ubora huu wengi unajulikana kama MOT.

Mafundi walioidhinishwa kufanya hiyo MOT hapa Uingereza wapo zaidi ya laki moja nchi nzima. Kampuni ya WTM Utility Services inachokifanya sio zaidi ya hiyo MOT.

MOT ya halali Uingereza inalipiwa paundi 45 tu. Hawa jamaa wa WTM Utility Services wanatoza paundi mia moja kwa kila gari! Huu ni utaratibu ambao haukubaliki.

Watanzania waishio Ughaibuni wana hamu na dhamira ya kuwekeza Tanzania taratibu kama hizi zinakwamisha na kupunguza dhamira yao hii. Sisi watanzania tuishio Uingereza hatuikubali hatua hii na tunaipinga:

ENDELEA KUISOMA NA KUSAINI PETITION HIYO HAPA:
http://www.ipetitions.com/petition/SAYNOTOTBSONTHISDUBIOUSDEAL/

No comments: