Thursday 14 June 2007

The Crooks


huyo pendeni ni mpambe, the BIG dad kulia mwa picha na instigator ni huyo wa kati. Kuibiwa wazi ndio huku. Sijui haya maamuzi wameyafanya wao tu. Ni swala la kujiuliza, hawa jamaa wamewahi kufika UK, kuona zoezi zima la MOT, garage zinazotumiwa kufanyia MOT na Maswali mengi tu ambayo wameshindwa kuyajibu.

Huu wizi, ujambazi wa BIG man with Suit, ni sawa au zaidi ya JAMBAZI mwenye kutumia silaha..

Majambazi haya yachunguzwe kisheria na ufanisi wao wa kazi.

KATU, DAIMA, MILELE hatutochoka kuwakemea kwa wizi na uzembe wa kikazi. Tupeni logic zenu mlizozitumia bado mko kimya. Siri kidogo kidogo itatoka, Subira zetu zinavuta Kheir. Hili changamoto ndio kwanza linaanza linaingia stegi mpya kabisa.

Eti wanasema wamelipa fees kubwa katika kujipatia hii tenda, ati ndio maana wanacharge zaidi ya MOT kulipa fidia zao. FEES kubwa ya nini ????? hiyo fees imelipiwa nini. Ni kitu cha kushangaza. Kampuni inashinda tenda au kutoa huduma kwa ajili ya serikali kwa sababu ya uhakika wa utekelezaji wao wa kazi, kwa kumaanisha vifaa vya kutosha, mafundi, na huduma bora.. sasa hili jiFEES latokea wapi.. Au ndio ujambazi wenyewe huo, tuliougusia hapo juu. Wananchi wapendwa hili swala tulikemee DAIMA DAIMA DAIMA, mpaka tuone nani ana neno la mwisho.

No comments: