Tuesday 5 June 2007

TAMKO RASMI TOKA CHAMA CHA SWAHILI UK


Hatimaye vijana waungwana uk, wameweza kukaa chini na kuongelea swala hili linalowagonga na kuwaumiza vichwa wengi hapa UK, ni vipi karne hii tuliyonayo bado tunakuwa na taratibu za udictator wa Mobutu na ukoloni mambolea. Wanyanyase wengi maslahi kwa wachache, soma zaidi toka blog ya saidi yakubu

Dhulma na makusudio haya gharamu yamewagusa wengi na kuwaumiza wengi, ushauri uliopo ni kwa manufaa ya wananchi na Tanzania kwa ujumla. WTM utility wajitoe katika zoezi hili kabla ya kujiharibia jina lao au hata kupoteza license yao ya kufanyia kazi hapa UK.

Kwa sababu the next step hawa vijana watakupandisheni mahakamani kwa kukiuka na kupinga taratibu zilizowekwa wazi na UK katika utaratibu mzima wa ukaguzi wa magari hapa nchini.
Na mambo ya kimahakama kama munavyoyafahamu, itabidi malawyer na maprosecutors wapitie utaratibu mzima wa WTM wa kazi na siyo MOT peke yake. Hilo pekee litakufikisheni pabaya, kwa hiyo ilani tunayokupeni achaneni na vigogo-TBS visivyofata sheria yao wenyewe huko Tanzania, mutakuja JUTA. Hii si Tanzania hii ni UK, Sheria ni msumeno. Hatutishani bali tunaambizana ukweli kwa sababu sote tunajaribu kulinda maslahi yetu wote ikiwa ya WTM na wafanyabiashara hapa nchini.

Ni mategemeo yetu mpira mutaucheza vizuri.

1 comment:

GAME THEORY said...
This comment has been removed by the author.