Saturday 16 June 2007

Barua ya Wazi kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Mheshimiwa Rais, hii ni barua ya kuelezea malalamiko yetu watanzania juu ya utendaji wa kazi wa TBS (Tanzania Bureau Standard), kufuatia hatua iliyochukuliwa na TBS kuwazawadia WTM utility-http://www.wtmutilityservices.com/ zabuni ya ukaguzi wa magari yanayosafirishwa toka Uingereza kupelekwa Tanzania.

Muheshimiwa rais mengi ya malalamiko na maswali muhimu yameulizwa na wananchi, juu ya zoezi hili zima la ugawaji wa hii zabuni ambao umeenda kinyume na taratibu nzima za ugawaji wa zabuni hiyo. Baadhi ya sehemu ya hayo malalamiko yameelezwa wazi katika blog za wananchi, ambazo inaonyesha wazi malalamiko na kutoridhishwa kwao.

Kama utapata fursa pitia.

http://wemsas.blogspot.com/ Jumuiya ya Waswahili UK

http://www.tzcommunity.co.uk/ Jumuiya ya Watanzania UK

http://saidiyakubu.blogspot.com/2007/06/katika-taarifa-kwa-vyombo-vya-habari.html

http://tbswtmuncovered.blogspot.com/2007/06/tamko-rasmi-la-wtmtbs-uncovered.html


Muheshimiwa Rais, lazima ifahamike sisi wananchi hatuendani kinyume na taratibu za kudhibiti ubora wa magari au bidhaa nyengine zozote zinazoingizwa nchini toka nchi za nje, tunalopingana nalo ni ubora wa maamuzi ya TBS na ile kampuni iliyozawadiwa zabuni ya kufanya zoezi hilo, WTM utility

Muheshimiwa rais, kwa ufupi huku Uingereza, kipo kitengo maalum ambacho kinaangalia na kuongoza zoezi zima la ukaguzi wa magari madogo na makubwa(malori), kitengo hiki cha serikali kimeweka taratibu, njia na misingi kabambe ambayo kampuni ya WTM utility pekee haina au haiwezi kutimiza au kufikia viwango hivyo muhimu vilivyotolewa na VOSA-Vehicle and Operator Services Agency. Kitengo hiki maalum cha serikali ya Uingereza kinasimamia sehemu moja ya ubora wa magari yaliyo barabarani Uingereza kwa ujumla http://www.vosa.gov.uk/, au kwa jina maarufu inaitwa MOT.

Muheshimiwa rais, kitengo hiki cha serikali kinatoa vibali maalum kukagua magari kwa maelefu ya garage huko UK, ambayo idadi yake hadi kufikia mwaka jana ni 18300, ambavyo vinaendana na kanuni, ziliwekwa wazi kabisa kuhusiana na uangalizi wa magari yote Uingereza chini ya uangalizi wa kitengo hiki cha serikali- VOSA.

Swala la kujiuliza muheshimiwa Rais hawa WTM utility, wana garage moja au mbili katika nchi nzima ya Uingereza, na vile vile wanadai wanahimili mobile Units ambazo pia zitatumika katika zoezi hili la ukaguzi wa magari, hii peke yake inaenda kinyume na sheria na kanuni za sehemu ya ukaguzi wa magari, zaidi pitia hii tovotu inayoelezea wazi ya hizo kanuni za ubora wa sehemu ya ukaguzi. http://www.transportoffice.gov.uk/crt/motgaragesandtesters/applyingtobeanmottestcentre/premisesspecification.htm

Muheshimiwa rais, haya ni maswali muhimu ambayo tunakuomba sisi watanzania tunaoishi huku Uingereza, kuwauliza hawa TBS.

Je waliweza kuwasiliana na VOSA au ministry of Transport UK na jumuiya ya wafanyabiashara Uingereza na Tanzania, kuhusiana na zoezi hili zima la ukaguzi wa magari, kwa sababu ya kuuliza swala hili muheshimiwa rais ni kwa ajili ya kufahamu kama haya maamuzi yamepitia moja ya vipengele vyao vya kisheria katika kufikia maamuzi ya swala lolote linalohusiana na utungaji wa sheria ya viwango.

QUOTE

Preparation of Standards

Tanzania Standards are the national documents prepared through consensus of all interested parties i.e. consumers, producers buyers, research institutions, etc standard specify inter alia quality requirements for final products, sampling procedures, test methods, labelling, and good manufacturing practices… UNQOTE

Soma zaidi kupitia huo mtandao hapo chini..

http://www.tptanzania.co.tz/tbs_body.html

Je ni vipi WTM wataweza kuitumikia nchi nzima Uingereza, katika zoezi hili, hali ya kuwa garage ya zaidi 18000, ambazo zimesambaa Uingereza nzima, ambazo pia ndio zenye kufanya zoezi hilo hilo ambalo litafanywa na WTM utility, peke yake wenye garage 2 na mobile unit moja tu ?

Muheshimiwa Rais, sisi kama watanzania http://wemsas.blogspot.com/ tunaoishi huku UK, wengi wetu tunamadhumuni makubwa kabisa ya kuiendeleza nchi yetu katika sekta za kibiashara (import/export) na uwekezaji wa vitega uchumi ndani ya nchi. Yote haya ni makusudio ya kuweza kujisaidia na kujikwamua kiuchumi sisi wenyewe binafsi, ndugu, familia na watanzania walio chini kimapato, hii yote ni katika juhudi za kupigana vita na umaskini kama ilivyoolezewa katika ripoti ya mkukuta. http://www.povertymonitoring.go.tz/#

Muheshimiwa Rais baadhi ya maelezo ambayo yameelezwa katika ripoti hiyo ya mkukuta moja wapo ni kipengele cha tatu Governance and Accountability. Mwenendo wa TBS unaenda kinyume kabisa na vipengele vyote vilivyoelezwa katika ripoti hiyo muhimu ya kuondoa umaskini. Muheshimiwa Rais, TBS inakiuaka na kuzorotesha juhudi za MKUKUTA, kwa hiyo basi inarudisha juhudi za wananchi walio wengi katika kujikwamua na umaskini.

Baadhi ya hivyo vipengele kutoka ripoti ya 2006 ni kama ifuatavyo.

Quote

MKUKUTA CLUSTER III: Governance and Accountability

Assessment of broad outcomes

Assessment of cluster goals:

GOAL 1 Structures and systems of governance as well as the rule of law to be democratic, participatory,

representative, accountable, and inclusive

GOAL 2 Equitable allocation of public resources with corruption effectively addressed

GOAL 3 Effective public service framework in place to provide foundation for service delivery improvements

and poverty reduction

GOAL 4 Rights of the poor and vulnerable groups to be protected and promoted in the justice system

GOAL 5 Reduction of political and social exclusion and intolerance

GOAL 6 Improve personal and material security, reduce crime, and eliminate sexual abuse and domestic

violence

GOAL 7 National cultural identities enhanced and promoted

Unquote

Muheshimiwa rais tunakwamishwa vibaya na vyombo vya serikali, kama hiki cha TBS, mstaafu mwenyekiti wa TBS hapo awali, Mwakyembe aliwahi kusema “TBS siyo jeshi la ulinzi la Polisi” ambapo baadhi ya hotuba yake ilitolewa na gazeti binafsi kwenye tovotu hii http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2007/03/26/87090.html

Maombi ya Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.

Muheshimiwa rais, tunachokiomba sisi wananchi tunaoishi huku UK, tunakuomba utumie fursa yako, kwa kuuunda tume maalum ya kujitegemea kuchunguza swala hili, kama hivyo itagua vigumu muheshimiwa rais tunakuomba kupitia taasisi ya kuzuia rushwa http://www.tanzania.go.tz/pcb/rushwa/majukumu.html, kuweza kulifikisha swala hili na kuchunguzwa ipasavyo.

Kwa kumalizia.

Muheshimiwa Rais Nitakupa hadithi moja NASA - National Aeronautics and Space Administration ya Marekani, walitumia karibuni milioni moja dola, kwa kufanya utafiti wa kalamu itakayotumika kwenye SPACE shuttle.. Russia waliamua kutumia PENCIL. Je hii habari inalingana na hii ?? Ni kitu cha kujiuliza.

Ni mahisio yetu serikali ingetamka rasmi kupitia TBS, kwamba gari yoyote inayotoka Uingereza, ambayo itatumika Tanzania lazima iwe MOT certified, hilo lingeeleweka wazi kabisa, wengi tungelikaribisha na kulihimiza.

Shukrani Sana kwa kuchukua ujumbe wetu, ni mategemeo yetu tutapata maamuzi ya haraka. Na vile vile tungependa kutoa pongezi zetu za wazi zikufikie wewe pamoja na utawala wako katika kuweka uwazi katika maamuzi ya kiserikali yanayohusu wananchi au nchi nzima kwa ujumla.

Daima tutatumia fursa hii kupitia tovotu yako maalum kuleta mapendekezo au hoja zetu pale inapotubidi tufanye hivyo.

http://www.jakayakikwete.com/tanzania/pages/Ask-the-President

Mungu Ibariki Tanzania.

Shukran!

No comments: