Sunday 10 June 2007

Tamko Rasmi la TBSWTM uncovered.

Usiri ndani ya taasisi na vyombo vya serikali Tanzania.

Ndugu wapendwa wananchi, hivi sasa tumeweza kuona usiri uliobobea katika swala hili, hakuna taarifa yoyote ya kuridhisha iliyotolewa, na TBS, au WTM ambayo yenye kujibu maswala na hoja zilizotolewa kutoka miongoni mwa community ya wafanyabiashara UK na Tanzania.

Ndugu wananchi umuhimu wa habari umekua ni mkubwa kabisa, kiasi ya kwamba taasisi na vitengo vya kiserikali hususan vya kitanzania zinashindwa au havina wasemaji wa kudumu ndani ya kampuni zao. Leo hii tumefanikiwa kuwa na mtandao, magazeti huru binafsi, na hata habari kwa simu ambazo zinawafikia wengi wa mamilioni ya watu ambao kabla ya miaka 15-20 iliyopita ilikua ni sehemu ambayo inamilikiwa na vyombo hivi vya serikali nchini Tanzania.

Ndugu wananchi, taasisi na vyombo vya serikali nchini Tanzania, bado viko katika usiri mkubwa kabisa katika kufanya maamuzi yanayowahusu wengi, haswa tukisoma katika hizi taratibu nzima za mikataba na njia nzima zilizotumiwa kuipatia WTM tenda hii muhimu ya ukaguzi wa magari hapa UK.

Ndugu wananchi tunakuombeni kampeni yetu tuzidi kuipeleka mbele, na tujonge ufanisi ambao utahitajika kuwezesha hili swala liwe katika vyombo vyetu vya habari, taasisi husika za kiserikali, kama vitengo vya kisheria vinavyotizama malalamiko ya rushwa au utendaji duni ndani ya sekta hizi muhimu za kiserikali.

Ndugu wananchi, mheshiwa rais Jakaya Mrisho Kikwete, ameweza kufahamu umuhimu huu wa habari, na yuko katika mbio za kujitahidi kulitumikia Taifa kwa kutumia vyombo hivi kupata habari na malalamiko muhimu kutoka wa wananchi wake. Tunawasihi tuitumie fursa hii muhimu kabisa tupeleke malalamiko yetu moja kwa moja kwa Rais kwa kutumia tovotu yake maalum kwa maswala kama haya.

Ndugu wananchi moja ya ufanisi huo ambao tuutumie katika kulisambaza kuielimisha jamii ya wafanyabiashara hapa UK na nchini, ni kama ifuatavyo.

  1. Ndugu waandishi wa habari Tanzania, jumuiya ya wafanyabiashara inaomba msaada wenu wa kupata habari muhimu kuhusu hili swala la mkataba mzima baina ya WTM na TBS. Sisi kama wananchi wenzenu tungependa kujua ukweli wa mambo, malalamiko yetu mengi tu kama mlivyosoma katika blog mbali mbali bado yameshindwa kutekelezwa au kujibiwa ikiwa ni TBS au WTM. Mpaka hivi sasa hatujapata majibu ya kuridhisha kutoka katika vitengo hivi. Tunawaombeni mtupatie majina ya wahusika wa hili swala, picha zao, wadhifa wao, na mikataba yao, au hata habari yoyote ile ikiwa ni ya rushwa, au ufisadi wowote ule ambao umepitika. Zawadi itatolewa kwa habari yoyote itakayoandikwa katika blog hii, kwa maelezo zaidi wasiliana nasi katika email hiyo hapo chini. Zawadi hiyo itajumuisha gharama zote za upatikani wa habari hizo.

  1. Hali kadhalika, ndugu wananchi waishio UK, tunaomba muweke jitihada zenu, katika kupata habari zaidi ya utendaji mzima wa kazi wa WTM, picha ya sehemu zao za kazi, na habari muhimu zinazotoka ndani ya WTM, kuhusiana na zoezi hili gharamu wanalolikusudia kulifanya.

Mwisho kabisa nawasihi, musiache kuweka kusajili sign zenu katika petition maalumu ya kupinga zoezi hili gharamu, na vile vile kupeleka kero, malalamiko, mawazo na fikra zenu kwa mheshimiwa rais Jakaya Kikwete.

Mungu ibariki Tanzania.

Taarifa hii Imetolewa na Wakereketwa. @ www.tbswtmuncovered.blogspot.com

2 comments:

Anonymous said...

Habari lazima tuwaletee waheshimiwa, tumechoka na vimbwanga vya wachache..

Anonymous said...

ongezeni Juhudi zenu