Saturday 28 July 2007

Bunge linaongelea swala zima la TBS Saga

Napenda kuwataarifuni effort na juhudi za http://www.tbswtmuncovered.blogspot.com/ na wadau wote walioshiriki katika kupingana na swala hili, limewezesha kufanikisha hili swala mpaka katika ngazi ya juu ya kiserikali.

Tunawashukuru sana gazeti la mwananchi kwa ujumla, hususan juhudi za wahariri kupokea malalamiko yetu, hadi kufikia kuchapisha barua ya wazi kwa rais katika gazeti lao, na kuwezesha kulifikisha kwa wabunge na viongozi wa ngazi za juu ndani ya nchi. Hatimae linajadiliwa bungeni.

Juhudi zetu, hatimae tunategemewa kufanyiwa kazi, kwa vitendo na siyo MANENO matupu.



Wakereketwa..

1 comment:

Simon Kitururu said...

Kazi nzuri Wakereketwa, matunda yanaanza kujitokeza.